Tuesday 31 May 2016

Hivi ndivyo alivyookolewa Alan Pulido

Image result for alan pulidoMamlaka nchini Mexico wameelezea namna mchezaji wa kimataifa Alan Pulido alivyookolewa baada ya kutekwa nyara mwishoni mwa juma.
Maofisa wanasema kuwa muda mchache baada ya kutekwa kwake Pulido alipambana na mmoja wa watekaji wake na kumyang'anya simu yake kisha akawapigia polisi.
Pulido, anayechezea klabu ya soka ya Olympiakos ya Ugiriki alijikata mkono wake wakati akijaribu kuvunja kioo kwenye mlango ili atoroke kabla ya polisi kuwasili katika eneo hilo.Alitekwa siku ya jumamosi na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao wakati akitokea kwenye sherehe moja karibu na mji wake anaoishi wa Ciudad Victoria katika jimbo la Tamaulipas.

Samatta aiongoza timu yake kucheza Europa

Mbwana samatta
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5­-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-­3.
Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2-­0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji.
Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis ambaye alifunga magoli matatu katika mchezo huo, na Sandy Walsh akifunga bao moja kabla ya Sporting Charleroi kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremy Perbet.
Kulingana na Mwananchi,Genk, ikicheza kwenye uga wake wa nyumbani wa Cristal Arena ilianza mchezo kwa kasi na dakika 16, ilipata penalti baada ya Samatta kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Nicolas Penneteau, ambaye alipewa kadi nyekundu

Monday 30 May 2016

Kauli ya JPM kujitoa sadaka yazua mjadala


Kauli ya Rais John Magufuli kwamba yuko tayari kuutoa mwili wake sadaka katika kupambana na rushwa na ufisadi uku kuwasaidia wanyonge, imeibua mjadala huku wanasiasa wakitofautiana.

Akizungumza katika Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema: “Unapoona watu wanashangaashangaa sana (ni) kwa sababu hawakuzoea haya. Na walifikiri nitakuwa part of them (sehemu yao), never (haitatokea), not me (si mimi).
“Ni mara 10 nisiwe rais, nikachunge hata ndege, nikakae kijijini kuliko niwe Rais halafu nivumilie uozo huu unaofanyika. I’m saying never (nasema haitatokea).”
Rais Magufuli amekuwa akizitoa kauli kama hizo mara kwa mara, hasa anapowawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali, huku ikidaiwa kuna upinzani mkali ndani ya chama chake cha CCM, hali inayohisiwa kusababisha kauli hiyo.

Mkurugenzi wa Fordia, Bubelwa Kaiza alisema kauli hizo za Rais Magufuli zinaonyesha uzalendo wa kweli na amefanikiwa kufanya mambo yaliyowashinda marais waliomtangulia.
“Ndani ya CCM kuna upinzani mkali kutoka kwa makada. Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita watendaji wa Serikali wamekuwa na mikakati ya kusaidia wezi na utapeli, hivyo anachofanya ni ‘revival strategy (mkakati wa kufufua),” alisema Kaiza.

Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu

Mpatanishi mkuu Syria
Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu katika kile anachosema kuwa, kuvunjika kwa mazungumzo ya amani, yenye nia ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano sasa.
Mohammad Alloush, anayetoka kwenye kamati kuu ya upatanishi HNC, amesema kuwa anajiondoa kwa sababu mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa mataifa huko Geneva, hayajazaa matunda au kutanzua matatizo wanayopitia raia wa Syria waliozingirwa na vita.
Kamati kuu ya mazungumzo hayo ya amani iliahirisha shughuli zake mwezi Aprili na hakuna tarehe ambayo imewekwa ya kurejelewa kwa mazungumzo.

Thursday 26 May 2016

Watanzania 8 waliotaka kujiunga na al-Shabab wakamatwa

BoinnetMkuu wa polisi Kenya amesema polisi pia wametibua shambulio la Islamic State
Serikali ya Kenya imefichua kwamba imewakamata raia wanane wa Tanzania waliokuwa katika harakati za kujiunga na kundi la wapiganaji la al-Shabab nchini Somalia.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari, polisi wanasema raia hao waliokamatwa katika kipindi cha miezi miwili iliopita walikiri kuwa mbioni kujiunga na kundi hilo la ugaidi.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu kuweka video mtandaoni likidai uwepo wa wapiganaji wa Kiislamu nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.

Klabu ya soka yafungwa mabao 44 Ecuador, Mchezaji afunga mabao 18 pekee

Pelileo Sporting ClubUwanja ulikuwa na mashabiki 200 wakati wa mechi hiyo
Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.

Mshukiwa wa ulipuaji Kampala apatikana na hatia

LuyimaMshukiwa mkuu wa mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa mjini Kampala mwaka 2010 amepatikana na hatia.
Isa Ahmed Luyima amepatikana na kosa la ugaidi.
Luyima alikuwa ameshtakiwa pamoja na washukiwa wengine 12 kuhusiana na mashambulio hayo yaliyosababisha vifo vya watu 74.

Monday 16 May 2016

Mikel Arteta kuondoka Arsenal

ArtetaArteta alijiunga na Arsenal 2011
Nahodha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuhama klabu hiyo majira haya ya joto.
Arteta pamoja na kiungo wa kati mwenzake Tomas Rosicky wanatarajiwa kuondoka baada ya mikataba yao kumalizika.

Sunday 15 May 2016

Tisho la bomu laripotiwa Old Trafford

Hofu ya kuwepo bomu uwanjani imesababisha mechi ya Manchester United na Bournemouth kuhairishwa.
Mechi ya mwisho katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old Trafford.
Kifurushi kinachoshukiwa kuwa na vilipuzi kilipatikana kimetegwa katika sehemu ya North West Quadrant.
Wachezaji wakiongozwa na kocha Louis Van Gaal walirudi kwenye chumba cha mabadiliko.
Tayari kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinajiandaa kuingia uwanjani baada ya kutajwa. Maelfu ya mashabiki waliokuwa wanasubiri mchuano huo walilazimika kutoka nje.

Saturday 14 May 2016

Lady Jay Dee Sasa Kuitafuta Haki yake Kwa Njia ya Mahakama.

Lady Jay Dee Sasa Kuitafuta Haki yake Kwa Njia ya Mahakama..Amtaka Gadner Kuomba Msamaha Mbele ya Umma la sivyo hatua za kumpeleka Mahakani zitaendelea, Soma Hii Hapa Chini:

Friday 13 May 2016

Serena William ala chakula cha mbwa

Serena William
Nyota wa mchezo wa tenisi kwa upande wa wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa baada ya kula chakula cha mbwa saa chache kabla ya kufuzu katika robo fainali ya mashindano ya Italian Open.
Serena alijaribu kula kijiko kimoja cha chakula cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani mwenzake Christina McHale katika seti za moja kwa moja.
''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande kimoja,kinaonja utamu'',alisema

Walimu walipwa vifaranga badala ya mshahara Uzbekistan

Walimu walipwa kuku kama mshahara
Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa. Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo.
Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka.

Zlatan Ibrahimovic kuondoka PSG

Zlatan Ibrahimovic
Mashambuliaji wa kiabu ya Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 inakamilika msimu huu na amehusishwa na uhamisho wa Manchester United,kilabu ya Los Angels Galaxy na AC Milan.
''Ninafurahia'',alisema.''Niliwasili kama mfalme na sasa naondoka kama kigogo lakini ntarudi''.
PSG imesema kuwa Ibrahimovic anaondoka kama mshambuliaji bora na mchezaji bora zaidi katika historia ya kilabu hiyo.
Ibrahimovic ameifungia mabao mengi zaidi klabu hiyo licha ya kujiunga nayo mwaka 2012 aiwa amefunga mabao 152 katika mechi 178.
PSG imeshinda taji la Ligue 1 kila msimu tangu Ibrahimovic ajiunge na kilabu hiyo.

Sunday 8 May 2016

SAMIA : Ukawa wananguvu kuliko wabunge wa Ccm

HATIMAYE Mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekiri kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekomaa.

Samia Suluhu Hasani, Makamu wa Rais wa Serikali inayoundwa na CCM amesema, upinzani una nguvu kubwa nchini na wabunge wa upinzani wamekomaa zaidi ya wa CCM.Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa ufunguzi mkutano wa UWT unaofanyika mjini humo katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

Msichana Asiye na Mikono Ashinda tuzo la Muandiko Bora

Anaya Ellick kutoka Chesapeake, Virginia hatumii viungo vya kumsaidia wakati anapoandika.

Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono.

Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema.

Akata sehemu za siri za mkewe ili apate mtaji

Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 , anadai kukatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Mashaka ili akauze Sh. milioni tano za Kitanzania akauze kwa mganga wa kienyeji ili apate mtaji.Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya,

Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.“ Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano

Saturday 7 May 2016

Mchezaji mwingine wa Cameroon afia uwanjani , Angalia VIDEO HAPA

 
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya soka barani Ulaya huenda utakuwa umekutana na taarifa za kusikitisha kwa taifa la Cameroon, usiku wa May 6 2016 Cameroon na Afrika  kwa ujumla ilipata taarifa za kushtusha, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa anaicheze Dinamo Bucuresti Patrick Ekeng.

Monday 2 May 2016

Diamond Azipangua Shutuma za Kutoka na Mrembo Lyyn..Adai Wanajaribu Lakini Zari Ndio Roho yake


Diamond Ameamua Kuwakata watu vidomo wanaosema kuwa yeye na Zari kwa sasa hakuna mawasiliano mazuri kisa mrembo aliyecheza kwenye video mpya ya Rayvan...kwa kumpost Zari kwenye page yake ya Instagram...Tetesi za Diamond kutoka na msichana huyo zimekuwa gumzo kubwa instagram ....

Roho ya SIMBA!!!.... wanajaribu ila hawatokaa Waweze... Nakupenda Mpaka Naugua! @Zarithebosslady 😙 #Mmechelewa

Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania

TrumpTrump alishambulia sana sera ya kigeni ya Obama
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.

Binti wa Obama, Malia kusomea Havard

Binti ya Obama, Malia kusomea Havard
Mwanaye rais wa Marekani Barack Obama,Malia,amefuzu kujiunga na chuo kikuu cha Havard.
Taarifa kutoka ikulu ya White House imesema kuwa Malia ambaye amekuwa mapumzikoni baada ya kuhitimu masomo ya chuo cha upili, atajiunga na chuo hicho cha kifahari mwakani.
Malia ataendelea na likizo yake kabla ya kujiunga na Havard mwakani.'' taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.

Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2% kutoka 11% hadi 9%

Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2%

Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaongezea wafanyikazi wote nchini humo asilimia mia mbili 2% mishahara.
Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.