Monday 2 May 2016

Binti wa Obama, Malia kusomea Havard

Binti ya Obama, Malia kusomea Havard
Mwanaye rais wa Marekani Barack Obama,Malia,amefuzu kujiunga na chuo kikuu cha Havard.
Taarifa kutoka ikulu ya White House imesema kuwa Malia ambaye amekuwa mapumzikoni baada ya kuhitimu masomo ya chuo cha upili, atajiunga na chuo hicho cha kifahari mwakani.
Malia ataendelea na likizo yake kabla ya kujiunga na Havard mwakani.'' taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.

Malia mwenye umri wa miaka 17 atakuwa anafuata nyayo za wazazi wake rais Obama na Mitchel ,ambao wote walihitimu na Shahada ya Sheria kutoka Kitivo cha Sheria cha chuo kikuu cha Havard.
Chaguo lake la chuo kikuu limekuwa likijadiliwa haswa na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
Malia ndiye binti wa kwanza wa rais Obama.
Binti mwengine wa rais huyo mwenye asili ya Kenya anaitwa Sasha na anaumri wa miaka 15.
 
Sasha na Malia Obama
Sasha anahudhuria shule ya upili ya kifahari ya Sidwell Friends.
Rais Obama amesema kuwa ataendelea kuishi mjini Washington Marekani hata baada ya kukamilisha kipindi chake cha urais wa Marekani hadi pale Sasha atakapotamatisha masomo yake ya shule ya upili.

No comments: