Wednesday 31 August 2016

Sheria tata za mtindo wa nywele katika shule za sekondari A.Kusini zasitishwa

Maandamano ya wanafunziWanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro.
Sheria kuhusu namna wasichana wa shule za sekondari wanavyochana nywele nchini Afrika Kusini zimesitishwa baada ya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliyofanywa na wanafunzi weusi, ameleza waziri nchini humo.
Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro.
Picha za mwanafunzi wa kike aliyeandamana kupinga sheria hiyo iliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ubaguzi, ambapo #AchaUbaguziKatikaPretoriaGirlsHigh ilitumiwa na watu zaidi ya mara 150,000 kwenye mtandao wa Twitter.


Maandamano ya wanafunzi 
Picha ya mmoja wa waandamanaji iliyosambazwa kwa maelfu ya watu kwenye Twitter
Sheria za shule zitasitishwa huku uchunguzi huru ukifanyika kuhusiana na madai hayo, amesema waziri wa elimu katika mkoa wa Gauteng.
Shule ya sekondari haijatoa kauli yoyote.
Kanuni kuhusu maadili ya shule hiyo ina orodha ya sheria kuhusu nywele, lakini haijataja mtindo wa nywele wa afro.
SOURCE : BBC

No comments: