Monday 5 December 2016

Dangote kuja kushitaki kwa Magufuli



Sakata la kusimama kwa uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha Dangote mtwara laja na sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho ALHAJ ALIKO DANGOTE kuamua kuja nchini kuonana na mkuu wan chi Mheshimiwa Dk John Pombe magufuli.
kwa taarifa tulizozipata mpaka sasa ni kwamba Mmiliki wa kiwanda hicho cha Dangote atakuja nchini kwa nia ya kuonana na Rais Magufuli ili kushtaki mambo kadhaa ikiwemo madai ya hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara
kiwanda cha dangote ndio kiwanda kikubwa zaid afrika mashariki kwa uzalishaji wa saruji kilisitisha uzalishaji wa sarujiwiki kama mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji mkuu wake Harpreet Duggal kuwa kiwanda kimeelemewa na gharama kubwa za uzalishaji

Kwa upande mwingine mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther  Baruti alitudokeza jana jion kuwa boss wake ameamua kupanga ziara ya kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wa dangote wa uzalishaji wa saruji ulio na dhamni ya zaid ya paundi million 500 za kimarekani
Aliendelea kueleza kuwa kuna mambo mengi tuliyokubaliana na serikali kabla ya kuamua kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hakuna tatizo na serikali maana imetupa msamaha wa kwenye kodi kwenye mambo mengi kuanzia kwenye mambo kama ardhi, mafuta ya dizeli lita million miatatu na mambo mengine mengi tu.

No comments: