Friday 10 February 2017

Freeman Aikael Mbowe amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Paul Makonda

Breaking News........

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10 February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.
Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).
Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudhalilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.
Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.

Mbowe ameendelea kusema " RC hana mamlaka ya kisheria ya kumuita mtu Polisi, nitamfungulia mashtaka ya kunichafulia jina langu kwa kunihusisha na biashara ya dawa za kulevya, nipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika.

Sisi kama Chama tunaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Serikali imechelewa kuendesha vita, CHADEMA na Kambi ya Upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila.

RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria.

Sjawahi kujihusisha kwa kufanya biashara wala kutumia madawa ya kulevya wakati wowote katika maisha yangu.

No comments: