Wednesday 12 July 2017

Tetesi za usajili leo tarehe 12.7.2017



Klabu ya Chelsea iliyo na maskani yake jiji la London imetuma ofa ya paund million 65 kwaajili ya kumsajili mshmbuliaji wa Borusia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gaboni.
Meneja wa Chelsea Antoni Conte ametuma ofa hiyo baada ya kukosa saini ya aliyekuwa mchezaji wa Everton Romeo Lukaku ambaye sasa amejiunga na mahasimu wao Manchester United jumatatu ya wiki hii. Mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo uekuja baada ya Chelsea chini ya meneja wake Conte kuonekana hana mpango na Diego Costa kwa msimu ujao ,Kwa Upande wa Dortmund wamefungua milango kwa mchezaji huyo kuuzwa , ripoti kutoka gazeti la “The Sun ” zineleza kuwa Pierre-Emerick Aubameyang anatamani sana kucheza ligi ya Uingereza. Aubemeyang aliibuka mpachikaji bora wa magoli katika ligi ya ujerumani msimu wa 2016/17, PSG na AC MILLAN pia zinafuatilia saini ya mchezaji huo kwa karibu zaidi

Tukiwa bado Stamford Bridge kocha wa Chelsea bado hajakata tamaa kuiwania saini ya mchezaji wa Real Madrid Alvaro Morata licha ya kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa PSG, Intermilan ,Ac Millan na Manchester United.
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ametangaza kuachana na mpango wake wa kutaka kumsajili kiungo wa Monaco Kylian Mbappe kutokana na ada kubwa ya uhamisho inayoitajika na Monaco hivyo ameeleza kuwa atamshawishi Mwenyekiti wa klabu hiyo Perez ili kukika nguvu zao kuipata saini ya Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard , akihojiwa na jarida laDiario Gol la nchini Uhispania ZInedine ameeleza kuwa anaamini watatumia uhaisho wa Morata kwenda Chelsea kama Chambo ya Kumpata Hazard
Klabu ya Man U imemweka sokoni mChezaji wake aliyekuwa anakipiga Sunderland kwa Mkopo Adnan Januzaj sokoni kwa dau la paundi Milion 10 , Inasemekana Januzaj anakaribia kutua Real Sociedad kwa ada ya Paundi milioni 10 kama man U walivyotangaza .
Klabu ya Man U licha ya kutishia kumwacha Mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic inatarajia kumwongezea mshambuliaji huyo mkataba wa muda mfupi kutokana na kuonekana afya yake imeimarika kiasi cha kuweza kurudi uwanjani , hata hivyo Zlatan Ibrahimovic alikwisha mkabidhi romeu Lukaku namba ya jezi yake.
Mchezaji wa Arsenal Oxlade-Chamberlain ameonekana akifanya mazoezi na klabu yake hiyo ya jijin London ingawa alikuwa anahusiswa na kujiunga na majogoo wa Liverpool
Klabu ya Portsmouth iemsajili Golikipa kinda wa Totenham Luke McGee (17), Luke alikuwa akichezea klabu ya daraja la kwanza Peterborough ambako alionyesha mawanikio makubwa na kujitwalia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika ligi hiyo.

No comments: