Wednesday 6 September 2017

Watoto wawili kati ya wanne waliokuwa wametekwa wapatikana wakiwa wamekufa

Wananchi wakishuhudia zoezi la uopoaji wa miili ya watoto wawili

ARUSHA: ​ Watoto wawili  Ikram na Maureen waliokuwa wametekwa wamepatikana katika shimo la choo ambalo bado halijaanza kutumika. Muda huu askari ndio wanafanya utaratibu wa kuwatoa.

Chanzo cha uhakika kinasema mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita kabla ya kukamatwa na kusema walipo watoto hao.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian huko Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari amethibitisha kutokea kwa tukio hili ingawa yeye kasema ni kisima.

Hapo awali Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.

No comments: